Taarifa Kuhusu Huawei HiSuite na Faragha
Huawei HiSuite ni bidhaa (au huduma) inayoendeshwa na Huawei Device Co., Ltd. na kampuni ambazo inazimiliki ulimwenguni (hapa ndani baadaye inarejelewa kama "Huawei", "nasi", "sisi", au "yetu") inayotoa urejeshaji na hifadhi rudufu ya data, sasisho la mfumo na uboreshaji kwa vifaa vyako vya simu. Tunaelewa umuhimu wa maelezo yako ya kibinafsi, na tutafanya tuwezavyo kuyalinda. Tunatoa ahadi kwamba tutachukua hatua mwafaka za usalama kulinda maelezo yako ya kibinafsi kulingana na viwango vya kawaida vilivyowekwa vya sekta.
Tafadhali soma na elewa Taarifa Kuhusu Huawei HiSuite na Faragha kabla ya kutumia bidhaa (au huduma) hii.
Hapa unawakilisha na kutoa hakikisho kwamba wewe ni mtu mzima unapoanza kutumia bidhaa (au huduma) hii. Ikiwa wewe ni mtoto, ni lazima mlezi wako akubali wewe utumie bidhaa (au huduma) hii na akubaliane na sheria na masharti husika.
Ikiwa una maswali, maoni, au mapendekezo yoyote, tafadhali wasiliana nasi kupitia laini ya simu ya moja kwa moja ya huduma kwa wateja: 400-830-8300/800-830-8300, kupitia huduma kwa wateja mtandaoni, au kwenye ofisi zetu kote ulimwenguni. Ili kupata orodha kamili ya ofisi zetu, tafadhali zuru ukurasa wa Wasiliana na Huawei.
Tuna idara (au wataalamu) inayoshughulikia ulinzi wa maelezo ya kibinafsi ambayo unaweza kuwasiliana nayo kwa kuzuru ukurasa wa Maswali ya Faragha.
Kwenye hali za kawaida, tutajibu ndani ya mwezi mmoja.
Ikiwa haujaridhishwa na jibu letu, hasa ikiwa unahisi kwamba usindikaji wetu au tunavyoshughulikia maelezo yako ya kibinafsi kunakiuka au kudhuru haki na/au maslahi yako ya kisheria, unaweza kutafuta suluhu kwingine, iwe ni kwa kuandikisha kesi katika mahakama ya watu ndani ya mamlaka husika, kuwasilisha lalamishi kwenye chama cha sekta kujidhibiti yenyewe au mashirika husika ya udhibiti ya serikali, au kwa mbinu nyingine.
1. Jinsi Tunavyokusanya na Kutumia Maelezo Yako ya Kibinafsi
Maelezo ya kibinafsi hurejelea maelezo mbalimbali yaliyorekodiwa kielektroniki au kivingine ambayo yanaweza kutumiwa kivyake au kwa mchanganyiko na maelezo mengine ili kutambua mtu fulani wa kawaida au kuangazia shughuli ya mtu fulani wa kawaida.
Maelezo nyeti ya kibinafsi yanajumuisha nambari ya utambulisho wa kibinafsi, maelezo ya bayometriki ya kibinafsi, nambari ya akaunti ya benki, maelezo ya mali, mahali mtu alipo, maelezo ya miamala, na maelezo ya kibinafsi ya watoto wa umri wa miaka 14 au chini.
Tutakusanya na kutumia maelezo yako ya kibinafsi kwa malengo yafuatayo tu ambayo yameelezewa ndani ya Taarifa hii:
Kukupa shughuli za kimsingi zifuatazo
(1) Hifadhi rudufu na urejeshaji
Ili kukupatia huduma za hifadhi rudufu na urejeshaji, tunahitaji kukusanya maelezo yako yafuatayo:
Maelezo ya kifaa, yakiwemo kitambuaji kifaa, mfumo endeshi, jina la kifaa, modeli ya kifaa, IP ya kifaa, na maelezo ya maunzi ya kifaa (kama vile modeli ya CPU na maelezo ya ROM/RAM).
Maelezo ya programu ya kompyuta, yakiwemo toleo la HiSuite na toleo la mfumo endeshi.
Data ya hapo kabla inahifadhiwa kienyeji tu na haitopakiwa kwenye seva za Huawei.
(2) Ukarabati na sasisho la mfumo la simu ya mkononi
Ili kukupatia huduma za ukarabati na sasisho la mfumo, tunahitaji kukusanya maelezo yako yafuatayo:
Maelezo ya kifaa, yakiwemo kitambuaji cha kifaa, jina la kifaa, modeli ya kifaa, modeli ya CPU ya kifaa, maelezo ya ROM/RAM, na toleo la mfumo.
Maelezo ya mtandao wa kompyuta, yakiwemo anwani yako ya IP.
Lengo la kukusanya maelezo haya ni kutoa toleo la ROM linaloambatana na kifaa chako.
Tutatumia maelezo yako ya kibinafsi kwa njia zifuatazo: Kutafuta na kusukuma toleo la ROM linalofaa la kifaa chako kulingana na maelezo ya kifaa na mfumo unayotoa, na pia kupakua ROM ya hivi karibuni zaidi na kusasisha mfumo wako baada ya kupata ruhusa ya kusuluhisha hatari zilizoko ndani ya mfumo.
Usipotoa maelezo haya, hatutoweza kusasisha mfumo wako ili kurekebisha hatari za kiusalama zilizopo.
(3) Masasisho na vipakuliwa vya programu
Ili kutekeleza masasisho na vipakuliwa vya programu zilizosakinishwa kwenye mfumo wako, tunahitaji kukusanya maelezo yako yafuatayo:
Maelezo ya programu, yakiwemo jina na toleo la programu.
Maelezo ya kifaa, yakiwemo kitambuaji cha kifaa na UDID.
Maelezo ya mtandao wa kompyuta, yakiwemo anwani yako ya IP na anwani yako ya Mac.
Lengo la kukusanya maelezo haya ni kutoa toleo la programu linaloambatana na kifaa chako.
Tutatumia maelezo yako ya kibinafsi kwa njia zifuatazo: Kutafuta na kusukuma toleo la programu linalofaa la kifaa chako kulingana na maelezo unayotoa ya mfumo, programu na kifaa, kupakua toleo la hivi karibuni zaidi la programu baada ya kupata ruhusa yako.
Usipotoa maelezo haya, hatutoweza kutafuta, kusasisha, na kupakua toleo la hivi karibuni zaidi la programu.
(4) Kuboresha huduma
Ili kukupatia uzoefu bora zaidi wa huduma, tunahitaji kukusanya maelezo yako yafuatayo: Takwimu ya programu na data ya tabia ya matumizi ya HiSuite. Lengo la kukusanya maelezo haya ni kutoa toleo la programu linaloambatana na kifaa chako.
Tutatumia maelezo yako ya kibinafsi kwa njia zifuatazo: Kukupatia uzoefu bora zaidi wa mtumiaji na huduma na bidhaa zilizobinafsishwa kulingana na takwimu za programu yako na data ya tabia ya matumizi ya HiSuite.
Ili kuanzisha au kukomesha kipengele hiki, wekea au ondolea alama Jiunge na mradi wa kuboresha uzoefu wa mtumiaji kwa kuenda kwa Mipangilio > Jumla ndani ya HiSuite.
2. Haki Zako za Mada ya Data
Unafaidika na haki za mada ya data kulingana na sheria husika. Ikiwa una maswali, maoni, au mapendekezo yoyote kuhusu haki za mada ya data yako, tafadhali wasiliana nasi kupitia maelezo ya mawasiliano yaliyoko ndani ya Taarifa hii.
3. Eneo na Kipindi cha Kuhifadhi Data
(1) Eneo la kuhifadhi data
Maelezo ya kibinafsi tunayokusanya na kuzalisha chini ya huduma za ukarabati na sasisho la mfumo za simu ya mkononi yatahifadhiwa kwenye seva zilizoko ndani ya Jamhuri ya Watu ya Uchina
(2) Kipindi cha kuhifadhi data
Tutahifadhi maelezo yako ya kibinafsi tu kwa muda unaohitajika kutimiza malengo yake, na tutafuta au kuondolea majina maelezo yako ya kibinafsi kupita muda uliotajwa hapo chini, isipokuwa ikiwa inahitajika kivingine na sheria na kanuni husika.
Kwa huduma za ukarabati na sasisho la mfumo za simu ya mkononi, kipindi maalum cha muda wa kubakishwa data yako ya kibinafsi ni kama ifuatavyo:
Data ya kibinafsi iliyotajwa hapo kabla itafutwa baada ya miezi sita (6) kuanzia siku ya mwisho uliyowasiliana nasi, sharti likiwa hakuna miamala ya kibiashara yaliyofanyika wakati wa kipindi hiki.
Kwa ziada, tukisitisha bidhaa au huduma zetu, tutakuarifu kwa njia ya taarifa ya msukumo, tangazo, au mbinu nyingine, na tutafuta maelezo yako ya kibinafsi au kuyaondolea majina ndani ya kipindi cha muda kinachoeleweka.
4. Masasisho kwa Taarifa hii
Huawei inabakia na haki ya kusasisha Taarifa hii mbeleni. Badiliko linapotokea, tutakutumia taarifa ya badiliko kwa njia ya kisanduku cha maelezo. Tutakusanya na kutumia maelezo yako ya kibinafsi tu kulingana na taarifa iliyosasishwa baada ya kupokea idhini yako.
Taarifa hii itaanza kutumika kuanzia tarehe ya sasisho.
Mara ya mwisho kusasishwa: Aprili 25, 2018
MUHIMU: Taarifa hii ya faragha inajumuisha taarifa ya faragha na kujitolea kwa programu ya Huawei HiSuite. Ili kujifunza zaidi kuhusu haki za mada za data, hatua za usalama wa maelezo, na maelezo mengine, tafadhali soma Taarifa ya Faragha ya Biashara ya Mteja wa Huawei.